30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili kufanya upasuaji wa masikio

Aminiel Aligaesha
Aminiel Aligaesha

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) ipo katika mchakato wa  kuanza kutoa huduma ya ubingwa wa hali ya juu kwa kufanya upasuaji wa kupandikiza sikio kwa watoto waliosumbuliwa na tatizo la usikivu.

Akizungumza na MTANZANIA jana hospitalini hapo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, alisema tayari Serikali imeshapeleka madaktari watano nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo.

“Tunatarajia kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kupandikiza sikio hapa Muhimbili hivi karibuni, madaktari wetu wapo nje ya nchi wakijifunza namna ya kufanya upasuaji huo,” alisema Eligaesha.

Alisema katika upasuaji huo, madaktari watakuwa wakiweka kifaa maalumu ndani ya sikio la mtoto mwenye tatizo la usikivu, ambacho kitakuwa kinamuwezesha kusikia vizuri.

“Muhimbili tunatarajia mapema wiki ijayo madaktari hao kuwa wamerejea nchini, pindi watakapowasili basi tutaeleza kwa kina jinsi upasuaji huo utakavyokuwa ukifanyika,” alisema.

Alisema Muhimbili itaanzisha huduma hiyo ili kuwezesha watoto wenye matatizo hayo kupata huduma kwa wakati.

Katika jarida la hospitali hiyo la Januari hadi Aprili, mwaka huu, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Dk. Edwin Liyombo, alinukuliwa akisema kuanza kwa upasuaji huo kutasaidia kuokoa fedha nyingi.

“Mgonjwa mmoja akipelekwa nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huu, hugharimu kati ya Sh milioni 85 hadi 100, kwahiyo matibabu haya iwapo yatafanyika hapa nchini, ni wazi kuwa tutaweza kupunguza gharama hizi kwa kiasi kikubwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles