24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

MUHEZA WADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM

NA AMINA OMARI -MUHEZA

WILAYA ya Muheza mkoani Tanga inadaiwa kupinga agizo la Rais Dk. Johm Magufuli la kutoa elimu bure baada ya kuanza kutoza    Sh 18,000 kama ada ya mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza.

Baadhi ya wananchi walitoa kero hiyo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu katika Kata ya Majengo.

Walisema   wamekuwa wakitozwa fedha hizo kwa kila mwanafunzi anayeandikishwa darasa la kwanza vinginevyo mtoto   hasajiliwi shuleni.

Mmoja wa wananchi hao, Happiness Swai, alisema dhana ya elimu bure imeshindwa kutekelezwa katika wilaya hiyo.

“Naomba kueleweshwa   maana ya elimu bure  kwa sababu  katika kata yetu shule zinachangisha fedha kwa ajili ya malipo kwa kila mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza ingawa tulielezwa na Rais kwamba ada zote kwa shule za serikali alikwisha kuzifuta,” alisema Swai.

Haruna Ramadhan alisema     awali walikubaliana katika kata hiyo kwamba kila mwananchi achangie Sh 5,000 za ukarabati wa miundombinu katika shule.

“Walimu tukiwauliza wanasema ni maagizo tumepewa na ofisa elimu kuchangisha fedha hizo hivyo hawana budi kutekeleza maagizo hayo kwa kumchangisha kila mtoto anayeanza shule,” alisema Ramadhan.

Baada ya kusikiliza madai hayo, mbunge alimuagiza Ofisa Elimu wa Shule za Msingi, Stuart Kuziwa kuyafanyia kazi madai hayo na kutoa majibu yatakayoweza kubainisha ukweli wa jambo hilo.

Hata hivyo,  Kuziwa alionyesha kushtushwa na taarifa hizo na kuahidi kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo kwa sababu tayari serikali inagharamia shule zake.

“Ninachojua michango iliyopo ni ya chakula ambayo tulikubaliana kuwa hiyo ni lazima kwa wazazi wote.

“Lakini michango mingine ni kuchangia tofali au Sh 5,000 kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule zetu,” alisema Kuziwa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles