30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MUHAS yajitosa uchunguzi ugonjwa wa ajabu

Profesa Ephata Kaaya
Profesa Ephata Kaaya

Na Gabriel Mushi, Dar es Salaam

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kinatarajia  kuufanyia utafiti   ugonjwa wa ajabu ulioibuka mkoani Dodoma   kupata suluhisho la ugonjwa huo.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Ephata Kaaya, wakati akifunga mkutano wa nne wa wataalamu wa sekta ya afya ulioandaliwa na MUHAS   Dar es Salaam.

Alisema chuo hicho kimekuwa kikifanya utafiti mbalimbali unaoisaidia serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya, hivyo ni jukumu lake  kuufanyia utafiti ugonjwa huo wa ajabu ulioibuka katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

“Tumepanga kuisaidia serikali kuufanyia utafiti ugonjwa huo kwa sababu umekuwa ukisababisha mtafaruku ndani ya jamii bila kufahamu chanzo chake halisi na hata suluhisho lake… Muhas tutaanza jukumu hilo hivi karibuni.

“Taifa hili bado linakabiliwa na matatizo ya afya na bila sayansi huwezi kuelewa mbinu za kutatua matatizo yanayotukabili, hivyo tutaendelea kufanya utafiti  kutatuta changamoto zinazoikabili jamii yetu,” alisema.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, John Michael, alisema tayari sampuli za ugonjwa huo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa   uchunguzi.

“Uchunguzi wa kina utakaofanywa na Muhas utaisaidia serikali kupata suluhisho lake kwa sababu sasa uchunguzi wa awali umeonyesha ugonjwa huo umesababishwa na sumu kuvu ambayo ni kemikali inayopatikana katika nafaka,”alisema.

Ugonjwa huo wa ajabu uliripotiwa kuibuka Juni 17 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu saba  na hadi sasa wengine 32 wamelazwa  katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa na ya Rufaa Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles