29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mufti Zubeir:Hijja mwaka huu ni kwa walio Saudia tu

Christina Gauluhanga, Dar es salaam

SHEKHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir, amesema kwa mwaka huu ibada ya Hijja haitakuwa ya waumini wote ulimwenguni, badala yake itaadhimishwa na watu waliopo Saudi Arabia, ikiwa ni sehemu ya kujikinga na virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mufti Zubeir alisema mahujaji waliokuwa wamejiandaa na safari hiyo watawasiliana na taasisi ya Hajji Mission Tanzania inayoshughulikia masuala hayo ili waone namna nyingine ya kufanya.

Alisema agizo hilo linatokana na msimamo wa Maulana wa Saud Arabia kufuatia kukithiri kwa janga la Covid 19.

“Mahujaji waliokuwa wamejiandaa watawasiliana na taasisi ya Hajji ili kuona cha kufanya,”alisema Zubeir.

Alisema msimamo huo ni sahihi kidini kwani ni fatea ya Maulamaa wa Fikhi tangu zama kwa lengo la kuhifadhia roho za watu pale ambapo utekelezaji wa ibada ya hija utapelekea roho za watu kuteketea kwa ugonjwa wa kuwaambukiza.

“Bakwata tunaunga mkono uamuzi huu hivyo waumini wetu wote wa hapa nchini hakutakuwa na fursa ya kutekeleza ibada ya hija mwaka huu, nawaomba wote wakubali kwa moyo wa kutishia na kuamini kuwa ni Kadar ya Mungu,”alisema Zubeir.

Wakati huohuo, Zubeir alisema kwa sababu ya kupungua kwa ugonjwa wa Covid 19 nchini madrasa zote zinaruhusiwa kuendelea na shughuli zake Kama ulivyokuwa  kabla ya ugonjwa huo. Alisema baraza la ulamaa ambaye ni mwenyekiti wake inatia ruhusa kwa sababu ya umuhimu wa ujenzi wa Imani unaoanywa na madrasa hizo nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles