24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

UVCCM wamjibu Membe kugombea urais

Ramadhani Hassan -Dodoma

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umemwambia  aliyekuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  na Waziri wa Mambo ya Nje katika awamu ya nne, Bernard Membe, aache maneno na kama anataka kugombea achukue fomu wakutane kwenye uchaguzi. 

Membe ambaye kamati kuu ya CCM imetangaza kumvua uanachama, Juni 21 mwaka huu, alipohojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW) kuhusu msimamo wake wa kugombea nafasi urais, alidai  dhamira yake ya kugombea bapo ipo.

 “Ni kweli kabisa mwaka huu nataka kugombea, kwa chama gani sijui, kwa sababu kama CCM ikinisafisha, naweza kugombea kupitia CCM, ni haki yangu, ni furaha yangu na furaha ya watu wengine kuona watu wakishindana,”alisema Membe.

Akizungumza juzi jioni jjini hapa Mwenyekiti wa UVCCM, Henry James, alisema kama Membe anataka kugombea achukue fomu wakutane kwenye koksi la kura.

 “Juzi nilikuwa nasikiliza chombo kimoja cha habari ametokea bwana mmoja anasema alikuwa kijijini kwao, huko anasema yeye atagombea na mimi nataka kumwambia kama anaona kugombea ni rahisi, gombea tukuone.

“Gombea halafu tukutane kwenye BOKSI la kura kama hujatoka manyoya, gombea tuone, hakuna haja ya kutisha watu kwamba nitachukua Jumatano, nitachukua Alhamis gombea,’ alisema James.

Alisema yeye akiwa kama Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wamejipanga kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo ikiwemo na nafasi ya Urais.

‘Na mimi kama Mwenyekiti wenu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi nataka niwaambie tumejipanga juu, chini, pembeni, katikati akija mgombea atakayeletwa na makaburu tutatandika, atakayeletwa na mabepari tutatandika, atakaeletwa na wababaishaji tutatandika, ataeletwa na hawa wanaojitengenezea kesi tutandika.

“Kwa sababu hoja tunazo, sababu tunazo na Watanzania wapo tayari kukichagua Chama Cha Mapinduzi,”alisema.

 “Na mbaya zaidi (Membe) anasema ndani ya CCM ana vigogo sita ambao wanamuunga mkono, chama hichi hakina vigogo wala vijiti, chama hichi ni cha wanachama.

‘Kwa hiyo kama kuna vigogo wanakudanganya kwamba kwa kuunga mkono kwamba utafika popote, wewe na vigogo vyako vyote chali hamtafika popote.

“Hii Nchi hatuwezi kuirudisha tulipokuwa, tumeishaamua kwenda mbele haturudi nyuma, kama kuna mtu anamashaka na uongozi wa Magufuli anyooshe mkono mungu amuone,”alisema James.

Katika hatua nyingine alisema wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu, ni vyema waliopo serikalini wakaacha kuwapa umaarufu viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwakamata.

“Mwaka huu wa uchaguzi kutakuwa na kelele nyingi sana na nyinyi mliopo Serikalini  Katambi ( Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ) acheni kuwapa  umaarufu hawa watu, hawa mnaowakamata wanaanza kulia, ni wajinga tu msiwape umaarufu.

‘Mwanasiasa mmoja amefanya ziara Dar es salaam hakukamatwa na mtu, amekwenda Pwani hakukatwa na mtu ameingia Lindi amefanya vituko pale amekamatwa   anasema Serikali inamuonea.

“Hivi Serikali kama inakuonea imekuacha Dar es salaam imekuacha Pwani eti ikakukamate  kule? Watanzania wanalazimishwa kuwa na huruma na watu wapuuzi sisi tunawaambia ni mwendo wa maendeleo tu na wale ambao wanadhani kwa kupiga kelele watabadilisha chochote naambia hawawezi.

Ingawa James hakumtaja mwanasiasa huyo, hivi karibuni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na viongozi wengine nane wa chama hicho, walikamatwa na polisi wakiwa Lindi na kuwekwa mahabusu kwa takribani saa 30 hadi walipoachiwa juzi.

Viongozi hao walikamatwa wakiwa kwenye mkutano wa ndani na kuelezwa sababu ni kufanya maandamano ya siyo na kibali ingawa juzi Zitto alisema mashtaka hayo yamebadilishwa na kuwa kutishia uvunjifu wa amani.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles