Mtumishi B arudi upya na ‘Mbingu’

0
509

Massachusetts, Marekani

Staa wa muziki wa injili kutoka Marekani, Mtumishi B, amerudi kivingine na video ya wimbo, Mbingu aliouachia hivi karibuni katika chaneli yake ya YouTube.

Mtumishi B, amesema video hiyo ni ya kwanza kwa mwaka huu na anaamini itawabariki watu wengi kwa sababu ya ujumbe uliopo ndani yake.

“Video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube, huu ni wimbo wenye kumsifu Mungu kwahiyo kila mtu anaweza kusikiliza na kubarikiwa, mashabiki wanaweza kuendelea kutazama video ya Mbingu kwenye YouTube na kunipa maoni ili huduma yangu izidi kukua,” amesema Mtumishi B.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here