29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MTU MWENYE KILO 588 ANAPOLILIA MLO MAALUMU

iMPIGA gitaa raia wa Mexico ndiye mtu mzito zaidi duniani akiwa na uzito wa kilo 588 au sawa na zaidi ya nusu tani.

Awali ilisemekana Juan Pedro Franco alikuwa na uzito wa kilo 501 wakati alipopelekwa hospitalini mapema mwaka huu.

Lakini sasa imebainika uzito wake ni kilo 588 na amekaribia kuvunja rekodi ya Manuel Uribe, raia mwenzake wa Mexico aliyefariki dunia akiwa na uzito wa kilo 597 mwaka 2014.

Juan Pedro alikuwa amepelekwa hospitalini kufanyiwa upasuaji utakaomwezesha kutembea kwani hajatembea kwa miaka sita baada ya awali kuomba msaada wa kupatiwa mlo maalumu vinginevyo angekufa.

Dk. Jose Antonio Casteneda, ambaye anamtibu alinukuliwa akisema itabidi awe akilishwa chakula maalumu kupunguza uzito wake kwa miezi mitatu kabla ya kumfanyia upasuaji, na kuongeza kuwa kuna matumaini watafanikiwa katika hilo.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32 alivuma zaidi mapema Novemba mwaka huu wakati picha zake zilipojitokeza mitandaoni zikionesha akitolewa nyumbani kwake katika jiji la katikati mwa Mexico la Aguascalientes. Alikuwa akisafirishwa kwenda hospitali iliyo umbali wa maili 100 mjini Guadalajara anakotibiwa.

Awali Julai mwaka huu aliomba msaada baada ya kusema wazazi wake hawana tena uwezo wa kugharimia chakula maalumu alichokuwa akitumia.

Na alisema kwamba hakuondoka katika chumba chake kwa miaka sita na alihofia kufa iwapo hatasaidiwa mlo huo maalumu.

Kuhusu matibabu anayopokea, mpiga gitaa huyu stadi alinukuliwa akisema ana matumaini ataweza kurejea hali ya kawaida ya kimaisha na kutumbuiza watu muziki.

Alikuwa na unene tangu akiwa kijana mdogo shuleni, lakini uzito wake uliongezeka zaidi wakati alipopata ajali akiwa bado katika ujana.

Ajali hiyo ilimweka kitandani kwa zaidi ya mwaka mmoja ikifuatiwa na kusumbuliwa na homa za nimonia hali ambayo ilichangia kasi ya kunenepeana kwake.

Vyombo vya habari vimemweleza kuwa ndiye mtu mnene anayeishi duniani kwa sasa kitu ambacho hakuna ubishani kuhusu uzito wake halisi.

Mwenzake Manuel Uribe alipoteza nusu ya uzito wake kwa msaada wa madaktari na wataalamu wa mlo baada ya kufikia kilele cha uzito wake.

Hata hivyo, Uribe alifariki dunia katika Jiji la Monterrey, kaskazini mwa Mexico Mei 26 2014.

Naye alipata msaada wa matibabu na mlo baada ya kuomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia gharama hizo ili arudie katika hali ya kawaida kwa vile naye alikuwa mtu wa kitandani.

Kitendo cha Mexico kutoa watu wanene zaidi duniani mfululizo hakishangazi kwani asilimia karibu 75 ya watu wake wazima wanahesabiwa kuwa wenye uzito mkubwa au wanene.

Hilo limesababisha taifa hili la Amerika Kaskazini kuwa moja ya viwango vya juu zaidi vya maradhi ya kisukari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles