27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mtoto aliwa na Simba

african_lion_king-wide_1

Na ELIUD NGONDO, SONGWE

WANANCHI wa Kitongoji cha Kikamba, Kijiji cha Itizilo Kata ya Ngwala Mkoa wa Songwe wameiomba Serikali kumsaka Simba ambaye amemuua mtoto, Shija Majaliwa (3).

Wakizungumza na MTANZANIA jana wananchi hao walisema mnyama huyo amekuwa tishio kubwa kwa kata nzima ya Itizilo hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi hao.

Wakizungumzia tukio la kuuawa kwa mtoto huyo, baba wazazi wa Shija, Majaliwa Ninchilo na Sara Petro walisema mtoto wao alikamatwa na Simba saa nane usiku baada ya kuingia ndani ya nyumba yao.

Wazazi hao walisema nyumba yao ina vyumba vya watoto ambapo walikuwa wamelala, lakini baada ya tembo kushambulia mazao yao mwanamume alikuwa  amekwenda kulinda shamba ambalo lipo mbali kidogo na nyumba yao huku mkewe naye akiwa kwenye shamba lingine lililopo jirani na nyumba yao.

Kwa kuwa alijiona yupo karibu, mama aliamua kutokufunga mlango wa chumba cha watoto ambapo akiwa huko shambani alisikia kishindo cha mlango ukifunguliwa na alipokwenda kuangalia alikuta mtoto huyo hayupo na alipochunguza aliona  nyayo za simba uwanjani.

Mama huyo alipiga yowe kwa kushirikiana na mumewe aliyerudi nyumbani haraka ambapo walianza kufuatilia kwa kushirikiana na majirani ambapo walisikia sauti ya simba akinguruma kichakani.

Kutokana na hali hiyo waliamua kuondoka kwa kuhofia usalama wao na kesho yake walikwenda katika eneo hilo na kukuta mabaki  ya baadhi ya viungo vikiwamo taya na mifupa ya kichwa pamoja na moyo.

Diwani wa Kata ya Ngwala, Donald Maganga (CCM) alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa kwa sasa shughuli nyingi za wananchi zimekwama kutokana na hofu ya kuvamiwa na simba

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles