33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MTATIRO AIVIMBIA KAMATI YA UTENDAJI WILAYA


Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, amesema Baraza Kuu la chama hicho ndilo lenye mamlaka ya kumhoji na si vinginevyo.

Mtatiro alisema hayo hivi karibuni alipozungumza na gazeti hili kuhusu taarifa za kuitwa na Kamati ya Utendaji ya CUF Wilaya ya Ubungo, kujibu tuhuma za kwanini yeye na baadhi ya wanachama wasifukuzwe kutokana na kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho.

“Nilisikia kuna viongozi wa Ubungo wanataka kunihoji, wananihoji vipi wa Ubungo wakati mimi kwangu ni Segerea? Mbali na hilo, mimi ni kiongozi na Baraza Kuu ndilo lina mamlaka ya kunihoji mimi. Vyombo halali vya chama havijaona wapi nimekosea,” alisema Mtatiro.

Mtatiro alisema kwa sasa chini ya uongozi wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad,  wanafanya kazi na hajawahi kuitwa kuhojiwa.

Gazeti hili pia lilimtafuta Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya ambaye alisema taarifa hizo hajazisikia bali zinaweza kuwa ngazi ya wilaya.

“Labda huko ngazi ya wilaya, lakini huku sijazisikia,” alisema Kambaya.

Desemba mwishoni mwa mwaka jana, gazeti hili liliandika kuwa Kamati ya Utendaji ya CUF Wilaya ya Ubungo iliwaita Mtatiro, Khalid Singano, Kassim Choga, Mawano Yusuf Kilemi, Jumanne Ally, Mwinyi Khamis na Twaha Rashid.

Katika taarifa hiyo, Katibu wa CUF wilaya hiyo, Ali Makwilo, alisema walioitika wito huo ni Katibu wa tawi la Kimara Stop Over, Yahaya Muhsin na Katibu wa Tawi la Matangini, Patrick Mwakasege pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles