27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtandao: Walioficha fedha nje wafichuliwe

Elias Msuya na mashirika ya habari
MTANDAO wa ONE wenye makao yake nchini Afrika Kusini umewataka Waafrika Kuungana na kutia saini azimio la kuitaka Benki ya Malipo ya Kimataifa (BIS)kuweka wazi taarifa za fedha zilizofichwa katika benki za nje ili kusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa.
Benki hiyo yenye makao yake makuu nchini Uswisi ilianzishwa tangu mwaka 1930 ikiwa na lengo la kuratibu benki kuu duniani katika kuzilinda kifedha na kukuza uhusiano wa kimataifa.
Benki hiyo sasa imetoa taarifa yake inayoeleza watu na makampuni yaliyoficha fedha kwa wizi au kwa ukwepaji wa kodi kutoka Afrika. Hata hivyo taarifa hiyo haikuwekwa hadharani.
Taarifa ya Mtandao wa Swiss Leaks ilisema hivi karibuni kwamba, Bara la Afrika hupoteza zaidi ya Sh trilioni 90 kila mwaka kutokana na fedha kufichwa katika benki za nje.
Tanzania ilitajwa hivi karibuni na mtandao wa Swiss Leaks kuwa nchi ya 100 huku kukiwa na Watanzania 99 walioficha zaidi ya Sh bilioni 205 katika benki za nje, hasa benki ya HSBC ya Uswisi.
Taarifa ya mtandao wa ONE imezitaka nchi za Afrika na wadau mbalimbali kupiga kura kuitaka benki hiyo kuweka wazi taarifa hiyo.
“Tusaidie kuifunua siri hii kuhusu ukwepaji wa kodi na kuweka wazi vitendo vya rushwa,” umesema mtao wa ONE.
“Rushwa, ukwepaji wa kodi na utoroshwaji wa fedha unagharimu maisha na mabilioni ya dola kila mwaka. Fedha hizo zinaweza kugharimia elimu, afya na huduma nyinginezo,” ilisema taarifa ya mtandao huo.
Lengo la mtandao huo ni kukusanya saini 100,000 na hadi jana walikuwa wameshakusanya asilimia 25 ya idadi hiyo.
Mtandao huo umezungumzia taarifa ya jopo la viongozi wa maendeleo ya Afrika iliyoweka wazi nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliyopoteza zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.3.
Fedha hizo ni mara mbili ya bajeti yake ya afya na elimu kati ya mwaka 2010 hadi 2012 zinazotokana na ukwepaji wa kodi katika migodi mitano kutoka makampuni ya kimataifa yenye uhusiano na visiwa vya British Virgin, kampuni iliyopo Bermuda, Jersey, Gibraltar na Ufalme wa Uingereza.
Mtandao huo umeongeza kuwa taarifa hizo zitasaidia dunia kuweka malengo ya kupambana na umasikini na kuhakikisha kuwa viongozi wanaleta maendeleo kwa kuwawezesha wananchi na kufichua rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles