23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

JK awataka wanafunzi kufaulu kwa akili zao

Pg 1Patricia Kimelemeta
RAIS Jakaya Kikwete amewataka wanafunzi wanaofanya mitihani kuhakikisha wanafaulu kwa akili zao na si kufaulishwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea vitabu milioni 2.5 vilivyotolewa na Serikali ya Marekani kwa wanafunzi wa sekondari nchini, Rais Kikwete alisema idadi kubwa ya wanafunzi nchini wana juhudi za kusoma, jambo ambalo limesaidia kuongezeka kwa ufaulu mwaka hadi mwaka.
“Hakuna mwalimu anayemsaidia mwanafunzi katika mitihani, kila mmoja anafanya kwa kutumia akili yake na juhudi zake, ndiyo maana ufaulu unaongezeka.
“Nimeshangaa kuona gazeti moja likiandika kuwa‘wanafunzi wamefaulu au wamefaulishwa? napenda nimjibu kuwa, wanafunzi wamefaulu kwa akili zao wenyewe.
“Kwa sababu wanasoma na wanabidii katika masomo yao, walimu wana moyo wa kufundisha ndiyo maana matokeo yameonesha wazi kuwa idadi ya ufaulu imeongezeka,” alisema.
Rais Kikwete alisema jitihada ya utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo nchini ni pamoja na kuwepo kwa vitabu vya kutosha shuleni vikiwamo vya masomo ya sayansi na hisabati ili kuhakikisha kuwa ufaulu unaongezeka.
Rais alisema kutolewa kwa vitabu hivyo kutasaidia wanafunzi wengi kupata vitabu vya kusoma ili kujihakikishia ufaulu.
Akizungumzia kuhusu malipo ya walimu alisema kila mwaka serikali imekuwa ikiongeza mishahara ya walimu ili kuhakikisha kuwa matatizo ya walimu yanapungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles