24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MSUVA: NATAMANI TUWE WENGI NJE

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ anayecheza soka la kulipwa katika timu ya Al Jadida Morocco, Simon Msuva, amesema anatamani kuona Tanzania ikitoa wachezaji wengi nje ya nchi.

Msuva, ambaye ameanza kwa mafanikio katika klabu yake mpya, Jumamosi iliyopita aliiwezesha Tanzania kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA kabla ya kuondoka kurejea Morocco, Msuva alisema kwa sasa hakuna kitu chochote anachoweza kujivunia, safari yake imeanza ila anatamani kuona Tanzania ikiwa na wachezaji wengi nje ya nchi wakicheza soka la kulipwa.

 “Kufanya vizuri kwangu ni sifa kwa nchi yangu, natamani kuona wachezaji wengi wakitoka nje ya nchi kucheza soka la kulipwa ili tuweze kuifanya timu yetu ya Taifa kuwa bora,” alisema.

 “Unajua tukiwa wengi na kufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri lazima mataifa tofauti yatamiminika hapa nyumbani kuchukua wachezaji, nchi yetu itafahamika,” alisema Msuva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles