SAFU ya ushambuliaji ya timu ya Barcelona inayotengeneza utatu wa MSN, ikiwa na maana ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar Jr, wanajifua kunoa makali yao katika upigaji penalti dhidi ya timu pinzani.
Safu hiyo imekuwa katika mazoezi makali ya kuhakikisha hawafanyi makosa wanapopata nafasi ya upigaji wa penalti hizo.
Kila mmoja kati yao ameonekana kuwa makini katika jambo hilo baada ya kuwa na uwiano wa kukosa penalti 10 kati ya 24 walizopata msimu uliopita.
Idadi hiyo ya penalti walizopata na kukosa inawafanya kuwa na asilimia 58 msimu uliopita.
Msimu huu Messi kapata mikwaju miwili ya penalti huku Neymar akikosa mmoja na kuwa na asilimia 75 za kupashinda penalti zao.
Kwa mujibu wa jarida la Marca, safu hiyo kwa sasa imeongeza umakini katika upigaji wao.
Messi ndiye mpigaji penalti wa kikosi hicho anapokuwa uwanjani hata hivyo wakati mwingine nyota huyo hubadilishana na Diego Alves ambaye hivi karibuni alipiga penalti dhidi ya Valencia pamoja na Manchester City.
Neymar na Suarez wanapambana ili kufanya vizuri katika upigaji wa penalti kabla ya Messi hajaamua kuhusu maisha yake ya baadaye.