23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Msichana anayevuja damu machoni

1458057017-marnie-rae-eye-bleeding-topLONDON, UINGEREZA

HUYU ni Marnie-Rae Harvey, ambaye hutokwa na damu machoni, lakini madaktari hawaelewi chanzo chake ni nini.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 anasema kuwa hawezi kutoka nje na hana marafiki kwa sababu kila mara huwa nyumbani kwao kutokana na hali hiyo.

Amewatembelea wataalamu wa macho, madaktari wa masuala ya uzazi, madaktari wa watoto na wataalamu wengine kujua sababu ya tatizo hilo.

”Inachoma na inapoziba jicho langu siwezi kuona,” alisema.

Hali hiyo isiyo ya kawaida pia huathiri masikio yake, pua, fizi, kichwa, kucha na ulimi.

Hali hiyo ilianza baada ya kijana huyo kutoka eneo la Stoke-on-Trent kuanza kukohoa damu mnamo Machi 2013.

Hali hiyo iliendelea kwa kipindi cha miaka kadhaa, hadi alipoamka usiku Julai mwaka 2015 na kujikuta uso wake umezibwa na damu, alikuwa akitokwa na damu machoni.

Wazazi wake waliita gari la kubebea wagonjwa na kumwahisha hospitali ambako daktari wa zamu alishangazwa na tukio hilo ambalo hawajawahi kuliona.

“Nilipokwenda hospitalini walichunguza macho yangu lakini kila kitu kilikuwa sawa. Nilifanyiwa uchunguzi wa damu na matokeo yake yalikuwa sawa,” alisema.

Kwa kipindi cha wiki mbili zilizofuata macho yake yaliendelea kutokwa na damu.

Marnie-Rae alifanyiwa ukaguzi mwengine, ambapo wataalamu wengi walibaini kwamba ana kinga zilizodhoofika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles