21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Shisha ni marufuku kwa wajawazito

OLYMPUS DIGITAL CAMERADUBAI, UAE

DUBAI imepiga marufuku wanawake wajawazito kuvuta ama hata kuingia katika migahawa inayouza shisha.

Hatua hiyo inafuatia shinikizo la kuimarisha afya ya umma na hasa afya ya mama wajawazito.

Sheria hiyo inawadia baada ya kampeni ya kuzuia wanawake wajawazito kuingia mahala panapotumika kuvutia shisha.

Kampeni hiyo inaendeshwa kwa kutumia mabango na picha ya mwanamke mjamzito akiambiwa na mwanaye aliyeko tumboni kuwa ”Uamuzi wa kuvuta au la ni wako si wangu”.

Mabango hayo yanaeleza kuwa watoto ambao hawajatimiza miaka 18 na wanawake wajawazito hawaruhusiwi kuvuta shisha au sigara.

“Kauli hiyo ni ya serikali, wala siyo hoja ya kujadiliwa na yeyote,” alisema Mkurugenzi wa Afya ya Umma wa Dubai, Marwan Al Mohammed.

Wamiliki wa kumbi za starehe zinazouza shisha wamekuwa wakilalamikia kutokuwepo kwa sheria zinazoharamisha wanawake wajawazito kuingia katika kumbi hizo.

”Sasa sheria hii inaweka bayana anayeruhusiwa kisheria kuvuta iwe ana pesa au la,” aliongezea kusema.

Mwaka 2014, milki hiyo ya Kiarabu ilipitisha sheria kali dhidi ya uvutaji wa sigara ambayo ilipiga marufuku matangazo yanayotangaza sigara.

Vilevile sheria hiyo ilipiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya gari iwapo mna mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles