25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MSHINDI WA TATU ALILIA BWENI TANGU CHEKECHEA

Na ELIZABETH HOMBO,

MAMA mzazi wa mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa Erick Mamuya, ambaye alijitambulisha kwa jina la   Kandida Simon, alisema mwanaye alikuwa akipenda shule kiasi cha kupelekwa shule ya bweni tangu akiwa chekechea kwa madai kuwa, anavyorudi nyumbani anachanganyikiwa na kushindwa kuelewa vyema masomo yake kwani shuleni anazungumza Kingereza na nyumbani wanazungumza Kiswahili.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mama wa mwanafunzi huyo aliyesoma Shule ya wavulana ya Marian iliyopo Pwani alisema. “Alipoanza kusoma chekekea alinidai sana nimpeleke boarding nikamwuliza kwanini anapenda bording, akasema anapenda kwa sababu akirudi nyumbani anawakuta dada zake wanaongea Kiswahili kwa hiyo wanapotezea malengo yake kwa vile shuleni wanasoma Kiingereza.

“Akaniambia mama ukinipeleka nakuahidi nitakuwa wakwanza, nikamwambia mwanangu wewe ni mdogo hata kujisafisha huwezi akasema mama nitaweza. Ikawa kama utani siku hiyo akaenda msalani kujisaidia akiniita mama njoo niangalie nimeweza kujisafisha.

“Binafsi roho ilikuwa inaniuma mtoto mdogo utampelekaje bording (bweni), akaenda hadi kwa mwalimu mkuu wake kuwa anataka bording baadaye nikaitwa na mwalimu mkuu akaniambia mtoto wako anataka bording, nikamjibu kuwa bado ni mdogo.

“Baadaye nikakaa naye nikamwambia akifika darasa la kwanza nitampeleka bording (bweni), akanielewa ndio nikampeleka mpaka alipomaliza darasa la kwanza na ile ahadi yake kuwa atakuwa wa kwanza akatekeleza mpaka anamaliza darasa la saba alikuwa akishika nafasi ya kwanza,”alisema.

Kwa upande wa Erick mwenyewe, alisema alitegemea kufaulu lakini si kwa kiwango hicho.

“Kikubwa ambacho kimenisaidia nifanye vizuri ni kumwomba Mungu na kujituma. Kwa mfano sisi shuleni kwetu saa tisa alfajiri tunaamka kusoma halafu tunakwenda kanisani kumwomba Mungu,”alisema Erick.

Alisema anakumbuka akiwa kidato cha tatu matokeo yake yalikuwa mabaya na alikuwa akiona uvivu kusoma lakini anawashukuru wazazi wake kwani walimsaidia cha kufanya.

“Wazazi wangu nao walichangia sana nifanye vizuri kwa mfano nikiwa kidato cha tatu matokeo yangu yalikuwa mabaya sana kupata A ilikuwa ni shida kweli kweli, kila nikitaka kusoma napata uvivu lakini baadaye wazazi wangu wakanikalisha chini wakanishauri kwa upendo nimshirikishe Mungu ili uvivu ninaoupata wakati nikitaka kusoma uishe,” alisema Erick.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles