Na MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM
MSHINDI wa shilingi milioni 20 za Biko kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Anthony Chitanda, amekabidhiwa fedha jana katika Benki ya NMB, Tawi la Bank House, Dar es Salam, sambamba na kupewa ushauri wa kifedha.
Chitanda aliibuka kidedea katika droo ya 30 ya Biko iliyochezeshwa Jumatano na kuvuna Sh milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji hao wa Biko, mchezo wa kubahatisha unaoendelea kutingisha katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema kwa kila anayecheza bahati nasibu yao, lazima ajiandae kulala masikini na kuamka tajiri.
Alisema ushindi wa Biko ni rahisi kwa wale wanaocheza kwa kutumia mitandao ya simu ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea Biko kikianzia Sh 1,000 na kuendelea.
“Mbali na kushinda Sh milioni 20 kama alivyoshinda Chitanda na hatimaye kumkabidhi fedha siku moja baada ya kushinda, pia Watanzania wanaweza kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh milioni moja, huku wanaocheza mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao wakiwa na nafasi kubwa ya kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili kuwania donge nono la Sh milioni 20,” alisema.