27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mshindi BSS kujulikana Januari 29

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mshindi wa Shindano la kusaka vipaji, nchini, Bongo Star Search (BSS) anatarajia kupatikana usiku wa Januari 29, mwaka huu jijini Dar s Salaam ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kiasi cha Sh milioni 20.

Shindano hilo litakalopambwa na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wakiongozwa na, Faustin Mfinanga, ‘Nandy’, Zuwena Mohammed, ‘Shilole’ na mmoja wa majaji wa shindano hilo, Christian Bella maarufu kama Mzee wa Masauti.

Akizungumza na Juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Benchmark na Muandaajiwa Shindano hilo, Rita Paulsen, ‘Madam Rita’ amesema kuwa mwaka huu shindano hilo litakuwa la kitofauti kuanzia washiriki hadi majaji.

“Tunamshukuru Mungu mwaka huu zawadi zitatolewa mapema, mshindi wa kwanza atapata kiasi cha Sh milioni 20, mshindi wa pili atapata kiasi Sh milioni tatu na wa tatu atapata Sh milioni moja,”amesema Madame Rita.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa, (BASATA) Augustino Makame amesema kuwa Waandaaji wameshakabizi zawadi za washiriki na sasa wanasubiri mshindi na kumwekea kwenye akaunti yake.

“Tunampongeza Madam Rita kwa jitihada zake katika kuinua vipaji na kusaidia vipaji vya vijana, tutahakikisha kila mshindi anapata zawadi kubwa zaidi na sio zawadi tu bali ni nafasi ya kuinua kipaji chake na kuishi ndoto zake,”amesema Makame

Aidha, ameongeza kila mtu ni mshindi na washiriki watakaoshindana ni wanne na wengine wawili wamepata bahati ya kuchaguliwa na mashabiki hivyo watakuwa jumla ya washiriki ni sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles