26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

TPDC yavunja rekodi ya uzalishaji gesi asilia

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania TPDC limevunja rekodi ya uzalishaji gesi asilia kutoka kiwango cha futi za ujazo milioni 150 -180  mwaka jana kwa siku kufikia futi za ujazo milioni 211 mwaka huu.

Akibainisha hayo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa mradi wa kuwaunganishia gesi wateja 506 wilaya ya kinondoni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio alisema uzalishaji huo unaenda  pamoja na ongezeko la mapato ya gesi.

“Kwa kipindi kifupi mapato katika mfuko wa mafuta na gesi nayo imeongezeka, kuanzia mwaka 2017 mpaka sasa tumechangia Sh. bilioni 208, katika umeme tumeendelea kuwa tunachangia kwa kiwango kikubwa sana, uzalishaji wa umeme sasa tunachangia takribani asilimia 60 ya umeme wetu unazalishwa kwa kutumia gesi  na unaingizwa katika gridi ya taifa,”amesema Dk. Mataragio.

Akizungumzia mradi wa usambazaji gesi majumbani, Dk.Mataragio anasema wateja 170 wataungaunganishiwa kata ya Sinza na wateja 336 watakuwa kata ya mgulani.

“Mtambo utakaofungwa katika maeneo haya utakuwa na uwezo wa kuwahudumia wateja 180 hivyo idadi ya ya wateja itaendelea kuongezeka kutoka 506 hadi 850 na mkandarasi amekwishapatikana,” amesema.

Amesema mradi huo utagharimu Sh bilioni mbili kwa ajili ya usambazaji wa gesi majumbani na mategemeo ni kumalizika ndani ya muda mfupi ujao huku mategemeo mradi huo utakapokamilika ni kufikia nyumba zaidi ya 1,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles