26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mshambuliaji wa Wolfsburg atoka jino uwanjani

WOLFSBURG, UJERUMANI

NYOTA wa klabu ya Wolfsburg, Adelino Freitas ‘Vieirinha’ juzi alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kutoka jino kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.

Katika mchezo huo wa hatua ya robo fainali ya kwanza, Wolfsburg walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kushinda mabao 2-0, lakini mchezaji huyo alitoka jino baada ya kugongana na Toni Kroos.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hakuwa na furaha, japokuwa timu yake ilifanikiwa kuwafunga vijana wa Zinedine Zidane na kusherehekea ushindi huo.

Wolfsburg wamejiweka katika mazingira mazuri ya mchezo wa marudiano ambapo watahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali.

Watu wengi walikuwa na imani kwamba Real Madrid wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo kama ilivyo kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou, ambapo Madrid ilishinda mabao 2-1 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mbali na mchezo huo, mchezo mwingine ambao ulipigwa juzi ni kati ya PSG ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Manchester City.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles