Prodyuza Deey: Wasanii msikimbilie majina ya studio

0
828

PRODYUZA DEEY (3)NA GEORGE KAYALA

PRODYUZA wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Lwambo ‘Deey’ amewashangaa wasanii wanaokimbilia studio zenye majina makubwa kwa imani ndizo zina uwezo wa kuandaa kazi zao vizuri kuliko studio nyingine.

Deey ambaye anamiliki studio ya Deey Record, iliyopo Mwembechai, alisema wapo maprodyuza wasio na majina makubwa lakini kazi zao ni bora kuliko wale maarufu.

“Nawashangaa baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kudharau studio za maprodyuza wasiojulikana licha ya kuwa na uwezo mkubwa huku wakikimbilia studio zenye majina makubwa ambapo baadhi yao hupata usumbufu mkubwa kiasi cha kukata tamaa,” alisema Deey.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here