25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Msanii wa Nigeria awatamani Ali Kiba, Diamond

Omo Alhaji YceeNA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa pop kutoka nchini Nigeria, Omo Alhaji Ycee, ametoa msaada wa Sh milioni moja katika kituo cha wanajamii cha Kigamboni Community Center (KCC) ili zisaidie kutokomeza umasikini.

Msanii huyo ambaye yupo katika ziara ya kutangaza muziki wake, aliliambia MTANZANIA kwamba ameamua  kuunga mkono kituo hicho kwa sababu  ya kujitolea  kwao kukuza vipaji na kuendeleza elimu kwa jamii.

Katika hatua nyingine, msanii huyo amedai atafanya mazungumzo na wasanii wanaofanya vizuri nchini katika muziki ili afanye wimbo wa kushirikiana.

“Wasanii ninaotamani kufanya nao wimbo ni Ali kiba na Diamond kwa kuwa wapo katika kiwango cha kimataifa,” alisema Ycee ambaye baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini ataelekea nchini Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles