32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Msalaba mwekundu watoa elimu kwa kamati ya maafa Kiteto

Mohamed Hamad-Manyara

Shirika la msalaba mwekundu, Tanzania Red Cross, limetoa elimu kwa kamati za maafa katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ili kukabiliana na majanga yanayoendelea kujitokeza kwa wananchi na kusababisha madhara makubwa.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Tumaini Magessa Meneja mradi wa usalama wa chakula Kiteto, Haruni Mvungi amesema kufufuliwa kwa kamati hizo kutapunguza adha na madhara kwa wananchi.

“Mafunzo yatajikita kuimarisha kamati ziwe tayari kukabiliana na majanga pia yatasaidia maeneo mengine ambayo hayajafikiwa na mradi huu kunusuru wananchi na maafa katika maeneo yao,” amesema Mvungi.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Tumaini Magessa amesema kamati hiyo itaondoa tuhuma dhidi yake kwa wananchi kuwa ndiye aliyekuwa na jukumu la maafa wilaya wakati ni mkurugenzi wa halmashauri na kuagiza uongozi huo kuhakikisha vijiji vyote 65 vya Kiteto vinapata elimu hiyo.

“Kwa miaka mitatu sasa Kiteto imekabiliwa na maafa tofauti, tulikuwa na Sumu kuvu watoto zaidi ya tisa walipoteza maisha, mvua kubwa imenyesha na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi yakiwepo maafa naamini kamati hii itakuwa mwarubaini kwetu,” amesema Magessa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Tamimu Kambona ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa Kiteto amelipongeza shirika hilo kwa kumkutanisha na kamati yake ambayo hawajawahi kukutanatoka iundwe.

“Tanzania Red Cross kufanya kazi Kiteto mimi mwenyekiti naonekana natimiza majukumu yangu, natamani mradi huu uwe endelevu na ufike kata zote lakini ninaamini kuna uwezekano wa elimu hii kusambaa maeneo yote,” amesema Kambona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles