27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi wa maji kunufaisha wananchi wa kata ya Issenye

Na Malima Lubasha, Serengeti

WANANCHI wa Kijiji cha Nyiberekera Kata ya Issenye Tarafa ya Grumeti wilayani Serengeti mkoani Mara, wameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia mradi wa maji ambao pindi utakapokamilika utasaidia kuondoka na kero hiyo ya kuchota maji ya madimbwi na visima tangu kijiji kianzishwe zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kijijij hicho, Nyiberekera Julius Maguha, Diwani Kata ya Issenye, Mossi Nyarobi wakati wa ukaguzi na ufuatiliaji mradi wa maji nyiberekera unaotekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilayani hapa kwa kuboresha kisima cha asili kwa njia ya kisasa.

Maguha amesema kisima hicho kimekuwepo hata kabla ya vijiji vya ujamaa wananchi walikuwa wanachota maji na wameendelea kuyatumia maji  hadi Machi 2023 ambapo Kampuni ya Grumeti Fund ilileta wazo la kuboresha kisima hicho ambapo walikuwa na mradi wa kuchimba visima virefu kwenye shule za sekondari.

Amefafanua baada ya kampuni hiyo ya Grumeti Fund inayojishughulisha na shughuli za utalii katika mapori ya akiba ya Grumeti na Ikorongo kuleta wazo hilo la mradi wa uchimbaji visima virefu vijijini kama kiongozi serikali ya kijiji walilipokea wazo la maji mserereko na kulipereka kwenye mkutano mkuu wa kijiji kuridhia maboresho ya chanzo hicho cha maji yanayofanyika sasa.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema kuwa maboresho ya maji eneo hilo waliwasilishwa RUWASA na serikali kutoa fedha kiasi cha Sh bilioni 1.3 ambazo zimetumika kuweka uzio, umeme, bomba la kuchuja na mtambo wa kusukuma maji kwenda kwenye tenki la lita laki tano,nyumba.

Aidha, kampuni ya Grumeti Fund awali wakiendelea na uchimbaji wa visima vijijini katika kijiji hicho ndio walijenga tenki la kupokea maji kutoka kwenye chanzo maji mserereko ambapo sasa wanapata maji safi na salama kwenye 30 vya kuchotea maji huku zaidi ya watu 450 wakituma maombi ya kuwekewa maji katika nyumba zao.

Amesesma kisima hicho kimekuwepo kwa muda mrefu hata kabla ya kuwa kiongozi watu kutoka  wilaya ya Bunda kijiji cha Kyandege walinufaika na kimbilio  wakati wa kiangazi na sasa kinahudumia na vijiji jirani vya Nyamisingisi, Singisi na Iharara (kata ya Nagusi) na kijiji mama Nyiberekera.

Aidha, Diwani Kata ya Issenye, Mossi Nyarobi amesemamradi wa maji kijiji cha nyiberekera kata hiyo imekuwa na changamoto ya maji safi na salama kwa muda mrefu baada ya chanzo kuboreshwa kuwa cha kisasa kuwekewa vifaa vya majimbubujiko muda wote wa masika na kiangazi yanapatikana  ameipongeza serikali kutoa fedha ambazo zimesaidia mradi huo kutekelezwa kwa kiwango kikubwa.

“Kulikuwa na changamoto eneo hilo kabla ya kisima kuboreshwa,gari lilipokuwa linapita karibu na chanzo hicho maji yaliacha kutoka hivyo kurudi baadaye hali hiyo ilirejea kama kawaida hivyo wazee waliamua kuhamisha barabara hiyo ipitishwe eneo jingine na changamoto haipo tena eneo limehifadhiwa vizuri kwa kupanda miti likiwa limezungushiwa uzio likilindwa ikiwemo kulifanyia usafi,” amesema.

Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Wilaya ya Serengeti, Mhandisi Deus Mchele, amesema baada ya kuanza kuboresha chanzo hicho cha asili kinaingiza maji lita 6,000 wakati wa kiangazi na masika lita 12,000 kwa saa kwenye tenki na kufafanua kuwa serikali imetoa fedha kutekeleza zaidi ya  miradi 20 ya maji vijiji mbali mbali wilayani hapo na nusu ya miradi inafanya kazi.

Amewataka viongozi wa vijiji na kata kulinda na kusimamia kwa kupiga marufuku shughuli za kibinadamu kufanyika katika chanzo hicho cha  maji nyiberekera kwa kukitunza kama makubaliano ya mkataba yalivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles