26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mr Blue: Nilimtoa mke wangu klabu za pombe

blueNA CHRISTOPHER MSEKENA

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khery Sameer, maarufu Mr. Blue, ameweka wazi namna alivyombadilisha kimaisha mke wake, Warda baada ya kumtoa kwenye klabu za usiku.

Mr. Blue, anayetamba na wimbo wa ‘Baki na Mimi’, alisema wimbo huo unaeleza maisha halisi ya yeye na mke wake huyo tangu walipokutana hadi walivyoishi na kufikia maamuzi ya kuoana na kuanzisha familia ambayo kwa sasa wana watoto wawili.

“Wimbo huu unagusa maisha ya mimi na mke wangu Warda kwa asilimia kubwa, wengi hawajui kuwa mke wangu nilikutana naye klabu mazingira ambayo wengi wanadhani si mazuri kwa mwanamke, lakini kwangu ni tofauti kwa kuwa mke wangu ana sifa zote za kuwa mke,” alisema Mr. Blue, ambaye yupo katika maandalizi ya kuweka wimbo huo katika picha za video.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles