Ben Paul: Tuige mfano wa 2Face, D Banj

0
763

benNA THERESIA GASPER

MSANII wa kizazi kipya, Bernady Paul ‘Ben Paul’, amewataka wasanii wa Tanzania waige tabia za wasanii wa Nigeria, D Banj na 2Face kwa kuwa huwa hawana masihara katika uandaaji wa kazi zao za muziki.

Ben Paul alisema wasanii hao wanajua wanachofanya kuanzia katika uandaaji wa kazi zao hadi jukwaani tofauti na baadhi ya wasanii wetu hapa hukurupuka bila kujiandaa kwa kazi zao.

“2Face na D Banj ni wasanii wanaoendelea kudumu katika muziki kwa miaka mingi kwa kuwa ni wahangaikaji na wana nguvu ya kifedha na kimuziki kiasi kwamba natamani siku moja nifanye nao kazi ya muziki,” alisema msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Sophia’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here