Mpalile: Miaka 14 kuchezea Tz Prisons imetosha

0
747

Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania Prisons, Lauriani Mpalile, ameamua kustaafu kuchezea kikosi hicho alichokitumikia kwa miaka 14 kuanzia leo.

Mpalile ambaye ni beki, amesema umefika muda sahihi wa kuwapisha vijana kuendeleza pale alipoishia, huku akiwashukuru wachezaji alioshirikiana nao katika kipindi chote tangu mwaka 2007.

“Nawashukuru wapenzi wote wa soka, waandishi wa habari na wadau wote tuliokuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha yangu ya soka, umefika muda sahihi wa kuwapisha vijana,” amesema Mpalile.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here