25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho kufungiwa michezo miwili

KOCHA wa Klabu ya Manchester United, Jose Mourinho
KOCHA wa Klabu ya Manchester United, Jose Mourinho

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, ana uwezekano mkubwa wa kufungiwa michezo mwili baada ya kocha huyo kuonesha utovu wa nidhamu kutokana na mchezaji wake, Paul Pogba, kuoneshwa kadi ya njano.

Manchester United juzi walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Trafford dhidi ya West Ham katika michuano ya Ligi Kuu ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Katika mchezo huo, nyota wa klabu ya Man United ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha duniani, Pogba, alioneshwa kadi ya njano na mwamuzi Jon Moss, kwa madai ya kujiangusha na kumdanganya mwamuzi.

Kitendo cha Pogba kuoneshwa kadi kilimfanya Mourinho amtupie lawama mwamuzi huyo, huku akionekana na hasira kali na kufikia hatua ya kupiga teke chupa ya maji ambayo ilikuwa pembeni mwa uwanja huo wa Old Trafford.

Kitendo cha Mourinho kupiga chupa na kumtupia lawama mwamuzi, kilimfanya atolewe kwenye eneo hilo ambalo makocha wanasimama na kutakiwa kwenda kukaa kwenye jukwaa.

Si mara ya kwanza kwa kocha huyo kupewa adhabu kama hiyo, ni mara ya pili sasa tangu amejiunga na Manchester United, huku mchezo wa awali akioneshwa kadi ni dhidi ya Burnley.

Baada ya kutolewa katika mchezo wa juzi, kocha msaidizi wa klabu hiyo, Rui Faria, alichukua majukumu ya Mourinho na kuwaeleza waandishi sababu za kocha huyo kushindwa kuongea baada ya mchezo kumalizika.

“Mourinho aliamini kuwa Pogba amechezewa vibaya na si kama mwamuzi alivyodai kuwa mchezaji huyo alijiangusha, lakini alishangaa kuona Pogba anaoneshwa kadi ya njano, lakini kila mmoja ameona kilichotokea kwenye tukio hilo la Pogba, ila mwamuzi ni msemaji wa mwisho,” alisema Faria

Kutokana na hali hiyo, Pogba anatakiwa kuukosa mchezo mmoja ujao dhidi ya West Ham katika Kombe la EFL, wakati huo Mourinho akitarajiwa kupewa adhabu na Chama cha Soka nchini England (FA), kutokana na kitendo hicho.

Hata hivyo, mashabiki mbalimbali wa klabu ya Manchester United wameonekana kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwashambulia waamuzi na kudai kuwa wanamuonea kocha huyo.

Wamedai kuwa, wapo makocha wengi ambao wana tabia kama ya Mourinho, lakini hawatoi adhabu kama wanavyofanya kwa kocha huyo raia wa nchini Ureno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles