26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lwandamina atambua wachezaji Yanga

ocha mpya wa Yanga, George Lwandamina
ocha mpya wa Yanga, George Lwandamina

JENNIFER ULLEMBO NA THERESIA GASPER

MKURUGENZI wa benchi la ufundi la klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm, jana alifanya utambulisho wa wachezaji kwa kocha mpya, George Lwandamina, katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, siku ya jana ilitumika kwa utambulisho na mazoezi mepesi ya kupasha mwili.

Saleh alisema wachezaji ambao hawakuweza kuripoti jana, wataungana na wenzao waliotangulia katika mazoezi yatakayoanza rasmi leo.

“Leo (jana) ilikuwa ni siku ya utambulisho, Pluijm alikuwa akimtambulisha kocha kwa wachezaji ili wajuane vema.

“Mazoezi yaliyofanyika yalikuwa ni kupasha misuli tu na kuchangamsha mwili, ila programu rasmi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara itaanza kesho (leo),” alisema Saleh.

Wachezaji walioripoti mazoezini ni Amis Tambwe, Deusi Kaseke, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Juma Mahadhi, Vincent Andrew ‘Dante’, Haji Mwinyi, Mbuyu Twite, Matheo Antony na Deogratius Munishi ‘Dida’.

Wengine ni  Ally Mustafa ‘Barthez’, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Canavaro’  Godfrey Mwashiuya, Said Juma, Pato Ngonyani na Juma Abdul.

Wachezaji ambao wanatarajiwa kujiunga na timu hiyo leo ni Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Hassan Kessy na Beno Kakolanya, huku Vincent Bossou akiwa bado ana matatizo ya kifamilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles