23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nape aomba wadau kuwekeza michezoni

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnuye
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnuye

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnuye, amewaomba wadau kujitokeza kuwekeza katika michezo, kwa kuwa ndio nguzo muhimu  inayodumisha ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki.

Nnauye aliyazungumza hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kuiaga timu ya Bunge SC inayotarajia kuelekea jijini Mombasa, nchini Kenya Desemba 2, mwaka huu, kushiriki mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki, yanayofanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu yanatarajiwa kuanza Desemba 4 hadi 14.

“Ukiachana na siasa, jambo lingine linalounganisha nchi hizo ni michezo, hivyo ni muhimu wadau kujitokeza kutumia fursa hii ili kuisaidia timu ya Bunge kushiriki vema mashindano hayo, kwani tuna uhakika itafanya vizuri,” alisema Nnauye.

Naye Mwenyekiti wa timu hiyo, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja, alisema wana uhakika wa kufanya vizuri baada ya kujiandaa vema kwa kuweka kambi ya mwezi mmoja mkoani Tanga.

“Kutakuwa na michezo ya aina sita ambayo yote tutashiriki, ukiwemo soka, mpira wa pete, wavu, riadha, kuruka kamba na gofu, lengo ni kudumisha  ushirikiano wa nchi washirika,” alisema Ngeleja.

Ngeleja alizitaja nchi sita zitakazoshiriki ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi na Rwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles