25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Izzo B: Sijawahi kufikiria kuacha muziki

MSANII wa hip pop, nchini, Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’
MSANII wa hip pop, nchini, Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’

Na THERESIA GASPER -DAR ES SALAAM

MSANII wa hip pop, nchini, Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’ ameweka wazi kwamba, hafikirii kuacha muziki hata atakapozeeka, kwa kuwa ndiyo maisha yake kwa sasa.

Izzo B aliliambia MTANZANIA kwamba, muziki ndio unaofanya maisha yake yawe alivyo sasa, hivyo hawezi kuacha muziki kwa kuwa ana historia nao na anauheshimu na ataendelea kuuheshimu hadi mwisho wa maisha yake.

“Naamini kwa kujituma zaidi kunaniongezea mashabiki wengi, naufurahia muziki wangu na napenda mashabiki wangu waendelee kuufurahia, hivyo nitajitahidi kuendelea kuwafurahia hadi nifikie mwisho wa maisha yangu,’’ alieleza Izzo B.

Izzo B kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Dangerous Boy,’ kupitia kundi lao la ‘The Amaizing’, ambao wapo mbioni kuachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Milele’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles