26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Moto wateketeza Bweni la wanafunzi shule Sengerema

Na Anna Luhasha, Sengerema

Wanafunzi wa shule ya Seminari wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamenusurika kifo baada ya Bweni lao kuteketea kwa moto wakati wakijisomea darasani usiku.

Akizungumzia tukio hilo Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Faravian Kasala amesema tukio hilo limetokea Juni 13, mwaka huu saa tatu usiku shuleni hapo.

Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Faravian Kasala.

“Nilipigiwa simu na Msimamizi wa shule wakati nipo Geita, akanitaarifu kuwa bweni limeungua, lilikuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 55 liliteketea lote, magodoro vitanda na vifaa vya wanafunzi,” amesema Baba Askofu Kasala.

Aidha, Baba Askofu Kasala amelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Sengerema kwa kufika kwa wakati eneo la tukio na kudhibiti moto huo.

“Nitumie nafasi hii kuwashukuru kamati ya ulinzi na usalama wilaya pamoja na Zima moto kwa kufika kwa wakati eneo la tukio na niwataarifu kuwa masomo yataendelea kwani shule inamiundombinu ya ziada,” amesema.

Aidha, amewaomba wadau mbali mbali nchini kuguswa na tukio hilo ambapo amesema mlango wa kusaidia upo wazi licha ya tasisi hiyo kutoa baadhi ya mahitaji kwa wanafunzi wake.

Upande wao baadhi ya wanafunzi akiwemo Mwenyekiti wa wanafunzi shuleni hapo, Emmanuel Mgonja wamesema wakati wakijisomea walisikia kelele kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ndipo walitoka madarasani na kuona moto unawaka juu ya paa ya bweni na kuanza kuuzima kwa kutumia vizimia moto vilivyopo shuleni hapo.

Nae Kamanda wa Zima moto na Uokoaji wilayani Sengerema ambaye pia ni Mkaguzi Msaidizi, Juma Ngwebe, amesema alipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa uongozi wa shule hiyo saa mbili na nusu usiku nakwamba walifanikiwa kuudhibitinakwamba hakuna mwanafunzi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana na uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani ya mali zote zilizoteketea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles