24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kampeni ya mjue jirani yako kudhibiti wahamiaji haramu

Na Ashura Kazinja, Morogoro.

JESHI la Uhamiaji Tanzania limeanzisha kampeni ya ‘Mjue jirani yako’ ili kutoa elimu kwa jamii juu ya namna ya kukabiliana na wahamiaji haramu na kuepuka madhara yanayoweza kutokea baadae kwa jamii au hata kuhatarisha usalama wa taifa kwa ujumla.

Kampeni hiyo inamtaka kila mwananchi kumjua jirani yake na kuepuka kukaribisha wageni au watu wasiofahamika na kuishi nao katika maeneo yao bila kujua undani au madhumuni yao ya kuwepo hapo, bila kutoa taarifa kwa uongozi husika hatua itakayokomesha uingiaji holela wa raia wa kigeni.

Akizungumza na juzi mjini hapa jatika mdahalo wa waandishi wa habari na wadau wa habari kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wa Mwandishi wa Habari mkoani hapa, Mrakibu wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania Mkoa wa Morogoro, Richard Sasongwe, amesema kampeni hiyo ya Mjue jirani yako itasaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa, pamoja na kudhibiti uingiaji holela wa raia wa kigeni nchini.

“Tuna kampeni kubwa ya mjue jirani yako, tunaenda kwenye vyombo vya habari, tunaenda mashuleni ili kuwaelimisha watu umuhimu wa usalama katika ngazi ya familia, kwani watu wengine sio wazuri, wengine wanakuja kutuchunguza, hivyo kunaweza kukawa na watu waliopandikizwa,” amesema Mrakibu Sasongwe.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji Mali mkoa wa Morogoro, Dk. Rozalia Rwegasila amewataka waandishi wa habari mkoani humo kuandika habari za kujenga mkoa pamoja na fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani humo, ikiwemo viwanda, madini, utalii, misitu, biashara na kilimo ili kuhamasisha wananchi wengi kwa maswala ya maendeleo.

“Tunataka mkoa wetu uendelee kwani kuna fursa nyingi za maendeleo, tunapenda kuona mnapotoa taarifa zenu mtoe zaidi taarifa za kuhamasisha maendeleo kwa wananchi, habari za kujenga mkoa, habari za fursa zilizopo kwenye mkoa wetu,” ameeleza Dk. Rwegasila.

Nae Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro, Ralph Meela, amesema kuwa ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari unaanza kwake mwenyewe kuhakikisha anajilinda kutokana na aina ya habari anazoandika pamoja na kupima kazi anayoenda kuifanya, ikiwemo kuepuka habari zitakazoleta taharuki kwa jamii au uongozi.

“Ulinzi wa Mwandishi wa habari unatakiwa unaanza na yeye mwenyewe, unatakiwa kujitambua kuwa wewe ni mwandishi wa habari na kujua hili ninalotaka kulifanya je litagusa upande gani, unatakiwa kupima uzito wa jambo unalotaka kuandika na athari zake,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles