Taarifa ya chama hicho imesema kwamba, wamechukua maamuzi hayo kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo pamoja na kukosekana kwa utulivu.
“Baada ya miezi 20 ya kukosekana kwa utulivu na matokeo mabaya ya timu, tumekubaliana kufikia mwisho wa mkataba na kocha wetu, Zaki.
“Tunaheshimu mchango wake katika kipindi hiki chote hadi hapa alipofikia, lakini kwa sasa hatuoni sababu ya kuendelea kuwa na kocha huyo na tayari tumemalizana, ila tunamtakia kila la heri katika maisha yake mapya ya soka kokote aendako,” lilisema shirikisho hilo.
Hata hivyo, Chama hicho kimesema kitatangaza kocha mpya wa kikosi cha timu ya Taifa siku chache zijazo, huku habari zikienea kwamba kocha wa zamani wa Ivory Coast, Herve Renard, anatajwa kama atakayechukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho.
Zaki, ambaye alikuwa ni kipa wa zamani wa timu ya Taifa nchini humo, mwenye umri wa miaka 56, alichukua mamlaka ya kuwa kocha wa timu hiyo kwa mara ya pili mwaka 2014, huku mara ya kwanza ikiwa mwaka 2002.