30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Blanc aongeza mkataba wa miaka miwili PSG

Laurent Blanc unfazed by not being Paris Saint-Germain first choice manager - videoPARIS, UFARANSA

KLABU ya Paris Saint Germain (PSG), imefanikiwa kumuongezea mkataba kocha wao, Laurent Blanc, ambao utamfanya akae kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2018.

Kocha huyo, ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa nchini Ufaransa, ameongeza mkataba huo wa miaka miwili baada ya mkataba wa sasa kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, kabla ya kocha huyo kuongeza mkataba mpya kulikuwa na taarifa kwamba kuna uwezekano wa kocha Jose Mourinho kuweza kujiunga na klabu hiyo mara baada ya kufukuzwa na klabu yake ya Chelsea, lakini kwa sasa kocha huyo ameweka wazi kwamba amemalizana na Manchester United, huku akitarajia kuanza kazi majira ya joto.

“Napenda kuishukuru klabu hii kwa kuendelea kuniamini na kunipa nafasi ya kuwa kocha wao kwa kupindi kingine cha miaka miwili, tangu nimeanza kuifundisha klabu hiyo mwaka 2013, nimekuwa mtu wa amani na furaha kutokana na kile ambacho kinaendelea.

“Nimekutana na wachezaji ambao wana vipaji vya hali ya juu na kunirahisishia kazi yangu, ninaamini nitaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu na kuifanya klabu hii kuwa klabu bora duniani kwa kutwaa mataji mbalimbali,” alisema Blanc.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Nasser Al Khelaifi, aliongeza kwa kusema kwamba, wamekuwa na furaha kubwa kuona kocha huyo akiendelea kuwa hapo kwa kipindi kingine cha miaka miwili, hivyo wanategemea makubwa kutoka kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles