24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MOI INA UPUNGUFU VYUMBA VYA UPASUAJI WATOTO

NA VERONICA ROMWALD- DAR ES SALAAM

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya upasuaji ili kutosheleza mahitaji yake.

Mkurugenzi wa MOI, Dk Respicius Boniface alikuwa akizungumza jana hospitalini hapo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kujitolea Duniani.

Alisema hivi sasa kuna vyumba sita pekee ambako pia alipokea msaada wa fedha  na vifaa mbalimbali  kutoka Taasisi ya Foundation for Civil Society (FCS).

“Kwa taasisi hii tunahitaji kuwa na vyumba angalau 15 ili kutosheleza na pia tunatamani tungekuwa na chumba kimoja kwa ajili ya watoto pekee, asilimia 60 ya wagonjwa wetu huhitaji upasuaji,” alisema.

Dk. Boniface alisema kutokana na hali hiyo wanalazimika kufanya upasuaji kwa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi    Jumamosi.

“Huwa tunawafanyia kati ya watoto 20 hadi 50 kwa siku na wakati mwingine tunalazimika kufanya hadi usiku,” alisema.

Hata hivyo aliishukuru serikali kuendelea kuijengea uwezo taasisi hiyo pamoja na wadau mbalimbali wanaoendelea kuisaidia ukiwamo Ubalozi wa Kuwait.

“Serikali ina nia ya dhati kuboresha sekta ya afya, wadau wakiwamo Jumuiya Khoja Shia Ithna Asher nao wamekuwa wakifadhili matibabu ya watoto na hadi sasa tumefanya kambi 20 na watoto 400 wamenufaika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles