Anna Potinus
Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa ameelezea maskitiko yake kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, Robert Mugabe aliyefariki nchini Singapore alikokuwa akitibiwa.
Rais Mnangagwa amethibitisha kifo cha Mugabe asubuhi ya leo Ijumaa Sepemba 6, kupitia ukurasa wake wa Twitter.
“Kwa masikitiko makubwa ninatangza kifo cha Baba wa Taifa na Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe,”
“Mugabe alikuwa ni nembo ya ukombozi ambaye alijitolea katika utafutaji wa kuwawezesha wananchi wake.
“Mchango wake katika historia ya taifa letu na bara zima kwa ujumla hauwezi kusahaulika kamwe. Apumzike kwa amani,” ameandika Mnangagwa.
Taaifa zinasema Mugabe ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1980 na kuondolewa madarakani mwaka 2017 alikuwa nchini Singapore kwa ajili ya matibabu tangu Aprili mwaka huu.