25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kambi ya Wanafunzi kidato cha nne yazinduliwa Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Jumla ya wanafunzi 1465 wa kidato cha nne katika mkoa wa Simiyu wenye ufahulu chini ya wastani wa alama 35 wameanza rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 lengo likiwa kuwasaidia waweze kufanya vizuri kwenye mtihani wa taifa ukaofanyika mwezi Novemba, Mwaka huu.

Wanafunzi hao kutoka katika shule mbalimbali za sekondari mkoa wameanza kambi hiyo rasmi leo mjini Bariadi ambayo imefunguliwa na Mkuu wa Mkoa Antony Mtaka ambapo kati ya hao wavulana ni 748 na wasichana 717.

Afisa elimu wa mkoa Erenest Hinju amesema kuwa wanafunzi hao wamepatikana baada ya mtihani wa utimilifu (Mock) mkoa uliofanyika mwaka huu ambapo wanafunzi wote waliopata chini ya D mbili ndiyo wamekusanywa kwenye kambi hiyo.

Hinju amesema kuwa lengo la kuwakusanya wanafunzi hao wote wenye ufahulu mdogo, ni kutaka kuhakikisha mkoa wa Simiyu kwenye mtihani wa taifa kidato cha nne hakuna mwanafunzi mwenye alama sifuri.

” Tuna uhakika kwenye kambi hii hawa wanafunzi wataongeza ufahulu kutoka hapa walipo, tumetafuta walimu mahili 63 ambao watafundisha masomo matano tu, Kiingereza, Kiswahili, Uraia, Historia na Biologia,” Alisema Hinju.

Aidha Afisa Elimu huyo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha na wanafunzi wengine wenye ufahulu wa juu 36 pamoja na wanafunzi wenye kutafuta kuongeza ufahulu 383.

” Kambi hii tumeitenga katika makundi matatu, wanafunzi wanaotafuta ufahulu zaidi, wanaotafuta kuongeza ufahulu pamoja na hao ambao ni wengi wanatafuta kufahulu jumla kambi ina wanafunzi 1884, ” amesema Hinju.

Mmoja wa wanafunzi hao wenye ufahulu wa chini Erick Mussa alisema walikuwa wamekata tamaa ya kusoma kutokana na matokeo hivyo kuletwa kwenye kambi itawasaidia sana kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mtihani wa taifa mwaka huu.

Kati ya walimu wanaofundisha kwenye kambi hizo, yupo mwandishi maarufu nchini wa vitabu Richard Mabala ambaye atafundisha somo la kiingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles