25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mmomonyoko wa maadili ni tatizo’

SARAH MOSES,-DODOMA.

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa, amesema kuwa mmomonyoko wa maadili umechangia sana kutozingatiwa kwa sheria,kanuni na miongozo mbalimbali katika utumishi wa umma.

Hayo aliyasema jana Jijini Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu ambapo alisema kuwa vita dhidi ya ukiukwaji wa maadili haviwezi kupiganwa na serikali peke yake.

“Ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa ,ubadhirifu na maovu mengine vinatokomezwa”alisema Majaliwa .

Alisema kuwa tatizo la mgongano wa maslahi ni kichocheo kikubwa cha ukiukwaji wa maadili, nakusema kuwa kinga yake ni kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za kazi kwa maslahi ya umma,mtumishi hana budi kuweka maslahi ya umma mbele kulikomasilahi yake binafsi.

“Mara kadhaa baadhi ya viongozi au watumishi wa umma wamekuwa wakifanya maamuzi kwa mambo wanayojua wazi kuwa wana maslahi binafsi nayo”alisema Majaliwa.

“Mfano katika halmashauri zetu wapo madiwani au watumishi wanaoshiriki kutoa uamuzi unaohitimishwa kwa kumpatia kazi mkandarasi au mzabuni wakati kampuni husika inamilikiwa na mwenza,rafiki,ndugu wa karibu au mtoa rushwa”alisema.

Vilevile alisema hali hiyo imechangia rasilimali za nchi kunufaisha watu wachache huku wananchi wengi wakiendelea kuwa fukara wakati wachache wakijitajirisha isivyo halali.

“Tutaendelea kuziba mianya,kwani tukiacha iendelee,itarudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kufikia dira ya maendeleo ya taifa pamoja na malengo ya maendeleo endelevu”

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Diwani Athumani alisema kuwa Afrika inapoteza mali nyingi kutokana na vitendo vya rushwa.

Nchi za Afrika zinapoteza Dola bilioni 50 kila mwaka kwa rushwa na asilimia 25 ya pato la taifa kwa nchi za Afrika zinapotea kutokana na rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles