27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Abiria wafurika, Taboa yaomba kusafiri saa 24

LEONARD MANG’OHA NA RAHMA SWAI (TSJ) -DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(Taboa), Enea Mrutu, ameiomba Serikali kuruhusu mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani kutembea usiku na mchana ili kukabiliana na wingi wa abiria katika msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Mbali na hayo alisisitiza kuwa endapo mabasi hayo yataruhusiwa kutembea usiku na mchana hakutakuwa na shida ya usafiri huku akitolea mfano kwamba hakuna sababu ya msingi kwa mabasi yanayotoka Mwanza kuzuiwa Morogoro na yale yanayotoka Dar es Salaam kuzuiwa Shinyanga.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mrutu alisema“Kwa mfano kutoka Shinyanga kwenda Mwanza kinachotakiwa pale ni kuongeza ‘patrol’ (doria) na kuhakikisha maeneo yote ya mizani kunakuwa na mtu wa kupima uzito wa magari na madereva wa mabasi na maroli kama wanatumia vilevi”.

Aidha Mrutu alipinga uamuzi wa Serikali kutoa vibali vya muda kwa mabasi madogo ili kusafirisha abiria kwenda mikoani katika msimu kama huu kwa kile alichodai kuwa hawana uzoefu wa kufanya kazi hiyo na mabasi yao hayajafungwa mfumo maalumu wa kudhibiti mwendo (GPS).

Kiongozi huyo wa Taboa pia alishauri kupunguzwa kwa vituo vya ukaguzi na ili kuondoa ulazima wa magari kuingia katika vituo vidogo hasa pale ambapo mabasi hayo hayashushi wala kupakia abiria ili kuokoa muda unaopotea pasipo ulazima wowote,

Kwa upande wake, Meneja wa Kituo cha Kikuu cha mabasi Ubungo (UBT), Imani Kasagala, alisema mwaka kuna viashiria vya idadi kubwa ya abiria wanaosafiri kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.

 “Leo ni theluthi ya kwanza ya mwezi, tofauti na miaka miwili iliyopita tayari tumeanza kuona ongezeko la abiria kwa hiyo tunafikiri mwaka huu abiria watakuwa ni wengi.

“Uhaba wa mabasi kimsingi haujakuwapo ila huenda kuanzia kwenye theluthi ya pili ya mwezi huu yaani Desemba 20 kukawa na upungufu, ingawa  Sumatra (Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini) wameshajiongeza zaidi wameshaanza kukaribisha wadau wanaoweza kuwa na vyombo vya usafiri ili viweze kukaguliwa mapema ili kukabiliana na adha,” alisema Kasanga.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles