24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mlundwa apata ‘shavu’ Kenya

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Bondia wa zamani na mwamuzi wa kimataifa nchini, Emmanuel Mlundwa, amechaguliwa kuwa mwamuzi wa pambano la ubingwa wa Jumuiya ya Madola linalotarajia kufanyika kesho Jumamosi Oktoba 2, 2021 nchini Kenya.

Kwa mujibu wa barua ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Kenya {KPBC}, Mlundwa atasimamia pambano hilo kati ya  Mkenya Sara Ochieng anayetetea ubingwa huo  dhidi ya Mmalawi Rucy Chisale.

 Tofauti na kuwa mwamuzi wa pambano hilo, Mlundwa ataendesha kozi ya waamuzi wa mchezo huo kwa siku kadhaa nchini humo ambayo itahudhuriwa na waamuzi kutoka nchini mbalimbali.

”Kamisheni inatambua  uzoefu wako katika ngumi, tunaomba pia  muda utakaokuwepo, uende kozi fupi  kwa waamuzi wetu  hapa Nairobi,” imesema barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Msaidizi wa KPBC, Julias Odhiambo.,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles