Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Bondia wa zamani na mwamuzi wa kimataifa nchini, Emmanuel Mlundwa, amechaguliwa kuwa mwamuzi wa pambano la ubingwa wa Jumuiya ya Madola linalotarajia kufanyika kesho Jumamosi Oktoba 2, 2021 nchini Kenya.
Kwa mujibu wa barua ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Kenya {KPBC}, Mlundwa atasimamia pambano hilo kati ya Mkenya Sara Ochieng anayetetea ubingwa huo dhidi ya Mmalawi Rucy Chisale.
Tofauti na kuwa mwamuzi wa pambano hilo, Mlundwa ataendesha kozi ya waamuzi wa mchezo huo kwa siku kadhaa nchini humo ambayo itahudhuriwa na waamuzi kutoka nchini mbalimbali.
”Kamisheni inatambua uzoefu wako katika ngumi, tunaomba pia muda utakaokuwepo, uende kozi fupi kwa waamuzi wetu hapa Nairobi,” imesema barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Msaidizi wa KPBC, Julias Odhiambo.,