32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mkwasa: Tutacheza kwa tahadhari

MKWASANEWNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa, amesema wanahitaji kucheza kwa tahadhari kubwa dhidi ya wapinzani wao Chad kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa  Jumatatu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars ilitarajia kurejea jana usiku baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Chad, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo wa kusaka nafasi ya kushiriki fainali za Mataifa Afrika (Afcon) mwakani.

Akizungumza kabla ya kuanza safari ya kurudi nchini, Kocha Mkwasa alisema  kuifunga Chad si rahisi kama watu wanavyodhani, hivyo wanahitaji kuwashambulia na kujilinda kwa tahadhari kubwa kwenye mchezo wao wa marudiano Jumatatu hii jijini hapa.

“Wametupa wakati mgumu mno kwenye mchezo wetu wa jana (juzi), wakatulazimisha kuachana na mfumo wetu tulioanza kuutumia kipindi cha kwanza na kutumia mfumo wa 5,3,2, ili kulinda bao letu na kuacha kusaka bao la pili baada ya kuona wanacheza kwa kupiga pasi ndefu,” alisema.

“Walitupa presha mno ila nilikuwa na wachezaji wazuri tulipata ushindi kwenye mazingira magumu kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya, mpaka tunamaliza mechi Kelvin Yondani alishikwa na msuli wa ajabu ulioanzia  kwenye mbavu hadi miguuni, hii nahisi ni kutokana na kukosa hewa hivyo kulazimika kukimbizwa hospitali,” alisema.

Mkwasa aliwaomba mashabiki kuendelea kuwasapoti kwenye mchezo wa marudiano, ili kuzidi kuwatia moyo wachezaji na kuendelea kufanya vizuri.

Kikosi cha Stars kitaingia moja kwa moja kambini Hoteli ya Urban Rose, Kisutu Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo wa marudiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles