22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Fufa: Abel Dhaira anahitaji maombi

Abel-DhairaNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la soka la nchini Uganda ‘Fufa’, limeeleza kushtushwa na hali ya mchezaji wa timu ya Taifa ya Uganda ‘Uganda The Cranes’, Abel Dhaira, anayeugua saratani ya tumbo likieleza wazi mchezaji huyo anahitaji maombi kwa sasa kutokana na hali yake.

Kipa huyo wa zamani wa timu ya Simba, alikutwa na maradhi hayo kwa mara ya kwanza Februari mwaka huu na kusababisha familia ya wapenda soka  duniani kushtuka.

Kwa mujibu wa taarifa ya Meneja Mawasiliano wa FUFA, Ahmed Hussein, ilisema baada ya kupata taarifa hiyo waliungana na kutoa taarifa kuwa wanaahidi kufanya kitu muhimu kwa ajili ya golikipa huyo aliyeitumikia Uganda kwa mafanikio.

“Kama FUFA tutawasiliana na wachezaji wa timu ya Taifa ambao kwa pamoja wapambane kwenye mechi hizi mbili dhidi ya Burkina Faso kwa ajili ya kumpa faraja golikipa huyu mwenye kipaji, ambaye aliwahi kuchezea timu za Express, URA, Simba (Tanzania) na IBV Vestmannaeyjar inayoshiriki Ligi Kuu nchini Iceland.

“Tuna huzuni kubwa juu ya hali ya sasa aliyonayo Dhaira, tuna imani Mungu wa mbinguni atamponya,” alisema.

Hussein alisema kuwa wachezaji wa Uganda watavaa fulana kabla ya mazoezi kumtakia apone haraka.

“Sisi kama familia ya Uganda Cranes, tunamuombea Dhaira apone haraka,” alisema.

Dhaira ni mtoto wa golikipa mkongwe wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya nchi hiyo, Bright Dhaira, ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa klabu moja inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Hata hivyo, kipa huyo ambaye familia yake imepanga kumfanyia maombi maalumu Ijumaa katika eneo lao la familia ‘Walukuba’ iliyopo mji wa Jinja, bado yuko kwenye mkataba na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Iceland, IBV Vestmannaeyjar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles