27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mkuu wa mkoa awapa somo wahitimu wa JKT

 

Na AMON MTEGA-SONGEA

Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuwa wazalendo ikiwa ni pamoja na kuzuia migomo mbalimbali inayojitokeza vyuoni.

Mndeme alitoa wito huo jana wakati akifunga mafunzo ya Operesheni Mirerani 2018 kwa vijana 1680 waliokuwa katika Kikosi cha 842 KJ Mlale, kilichopo Songea Vijijini, Mkoa wa Ruvuma.

“Kumekuwa na baadhi ya vyuo nchini kukabiliwa na changamoto ya migomo ya mara kwa mara, ambapo wanavyuo wamekuwa wakiharibu rasilimali za vyuo kwa kuwa wanavyuo si wazalendo.

“Kwa hiyo, kuanzia sasa vijana mliobahatika kupata mafunzo haya ya kizalendo, nendeni vyuoni mkaendeleze amani na muondoe migogoro ambayo imekuwa ikirudisha nyuma suala la maendeleo ya Taifa.

“Uharibifu wa mali unaofanyika vyuoni hauwezi kukubalika kwani ni kinyume cha sheria za nchi. Kwa hiyo, ni lazima vijana mkaibadilishe hiyo hali na kuliweka Taifa katika misingi bora,” alisema Mndeme.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Makao Makuu ya JKT, Kanali Abbas Ahamed Abbas, alisema wahitimu hao wamefundishwa maadili ya uzalendo ambayo wanaamini wakiyatumia vizuri yatasaidia uwepo wa mabadiliko ya tabia katika jamii.

Pamoja na hayo, Kanali Abbas aliwataka wahitimu hao kukemea vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa wazalendo.

Naye mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Elizabeth Hange, alisema mafunzo hayo yamewasaidia maana ya uzalendo na uwajibikaji kwa Taifa lao.

“Wengi wetu mwanzoni hatukujua maana ya uzalendo, lakini baada ya kupata mafunzo haya sasa tumeelewa na tuko tayari kuwaelimisha wenzetu ili waipende nchi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles