25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

MKUU WA MKOA ASIMAMISHA WATUMISHI

Na ALI BADI, LIWALE


godfrey-zambiMKUU wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amewasimamisha kazi watendaji watano kwa kushindwa kusimamia ipasavyo mali za Serikali na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni nane.

Kusimamishwa kwa watendaji hao kulitokana na malalamiko ya wananchi kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kibutuka, Wilaya ya Liwale juzi.

Akizungumza wakati akiwasimamisha watendaji hao, Zambi alisema alilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya watumishi hao kushindwa kuwajibika ipasavyo na kuwafanya wananchi washindwe kupata huduma ya upasuaji katika kituo cha afya kijijini hapo.

“Hasara iliyotokana na uzembe wa watendaji hao ilitokana na kutofuata utaratibu wa utunzaji na makabidhiano holela ya vifaa tiba na uliosababisha upotevu wa vifaa
tiba vyenye thamani ya shilingi milioni nane,” alisema Zambi.

Watendaji waliosimamishwa kazi ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Gaudence Nyamiula, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Dk. Martin Mwandike, aliyehamishiwa wilayani Kibiti.

Wengine ni Mfamasia wa Wilaya hiyo, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibutuka, Adorati Daudi na Ofisa Utumishi wa Wilaya, Mfaume Kassimu, aliyehamishiwa Wilaya ya Newala.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dk. Maulid Majala,
alisema halmashauri ya wilaya hiyo ilipata vifaa tiba kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya huduma ya upasuaji na kupelekwa katika Kituo cha Afya
Kibutuka, lakini havikufanya kazi kwa kuwa hakukuwa na chumba cha kuvihifadhia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles