25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano Mkuu TFF Des 19

21NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

MKUTANO Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unatarajiwa kufanyika Desemba 19 na 20, mwaka huu.

Kikao cha Kamati ya utendaji cha Shirikisho hilo, kilichokutana Septemba 6 mwaka huu kimepanga kufanyika kwa mkutano huo huku ajenda zake zitatangazwa baadaye.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema ajenda hizo zitatolewa kwa mujibu wa Katiba ya TFF.

“Tunawataarifu wajumbe wa mkutano mkuu tarehe ya mkutano ni Desemba 19 na 20,” alisema.

Wakati huo huo, TFF imezitaka klabu ambazo bado hazijawalipia wachezaji wao wa kigeni dola 2,000 kukamilisha zoezi hilo kabla ya kuanza Ligi Kuu, endapo watakuwa hawajakamilisha wachezaji hao hawataruhusiwa kucheza michezo wa Ligi Kuu, inayotarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu.

Klabu zote zinatakiwa kuwalipia wachezaji wao wa kigeni kiasi cha dola 2,000, sawa na Sh milioni 4 za Tanzania, ambapo wachezaji ambao hawajalipiwa hawatapewa leseni za kucheza Ligi Kuu.

“Ninaziomba klabu zote zikamilishe zoezi hilo na watumie siku hizi zilizosalia kuwalipia wachezaji wao, endapo ikifika hadi siku ya Jumamosi hawajalipiwa basi wachezaji hao hawataweza kucheza ligi hii hadi pale watakapofanyiwa malipo benki,” alisema.

Alieleza msimu huu wachezaji wa kigeni wapo 29, Yanga, Azam na Simba wana wachezaji saba saba kila timu, wawili kutoka Stand United, African Sports pamoja na Mbeya City wana mchezaji mmoja mmoja, wakati Coastal Union wana wachezaji wanne.

Aliongeza kuwa, Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera ambao unatumiwa na Kagera Sugar, hautatumiwa na klabu hiyo kwa raundi tatu za mwanzo ili kupisha ukarabati unaofanywa.

Alisema kuwa katika kutambua hilo, klabu ya Kagera Sugar itatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora hadi pale utakapokamilika uwanja huo.

Lakini viwanja vingine vyote vimepitishwa na shirikisho hilo, baada ya kukidhi mahitaji yake ambayo walikuwa wanayahitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles