24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Kerr awapa somo nyota wake

dylanker-haiphongNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Daylan Kerr, amewapa somo nyota wake kuhakikisha wanapeana maelekezo ya kiufundi wenyewe kwa wenyewe wakiwa dimbani, kwa lengo la kukabiliana na upinzani wa timu yoyote ili timu itoke na ushindi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kerr alisema ameamua kufanya mabadiliko kidogo ya ufundishaji, ambapo wachezaji wanaoonyesha kuelewa zaidi mazoezini, watakuwa na jukumu la kuwasaidia wanaoshindwa.

Kerr alisema muda uliobakia kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ni mdogo, licha ya kuwa watakuwa na nahodha, wachezaji wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu.

“Nimeamua kufanya hivi ili kusaidia kikosi changu, kila mchezaji atambue ana jukumu la kumuelekeza mwingine wasitegemee mafunzo ya mwalimu tu au maelekezo ya nahodha.

“Kama wachezaji watashindwa kushirikiana wenyewe kwa wenyewe, hakutakuwa na faida yoyote ya maandalizi tuliyofanya hadi sasa,” alisema Kerr.

Alieleza maamuzi yake ya kuwataka wachezaji wapeane maelekezo, yatamsaidia kila mmoja wao kutambua mapungufu ya mwingine.

Simba inatarajiwa kufungua msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuvaana na African Sports, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mkoani Tanga Jumamosi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles