Geneva, Uswisi
Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya VVU na UKIMWI (UNAIDS), Michel Sidibe, ametangaza kujiuzulu nafasihiyo ifikapo Juni, mwakani ambapo ni miezi sita kabla ya muhula wake kumalizika.
Sidibe, amefikia uamuzi huo baada ya jopo huru kusema uongozi wake una kasoro na umevumilia utamaduni wa manyanyaso ikiwa ni pamoja na manyanyaso ya ngono na matumizi mabaya ya madaraka.
Jopo la watu wanne waliwasilisha ripoti yenye kurasa 70 Ijumaa, iliyopita wakisema kwamba utamaduni wakupendelea wanaume katika eneo la kazi hali ambayo imeruhusu watu kutohofia kushtakiwa na kulipiza kisasi.
Taarifa ya idara hiyo ilieleza Sidibe, alitangaza uamuzi huo jana Alhamisi, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa bodi ya UNAIDS ambayo ilikuwa inapitia ripoti yajopo hilo.
Sidibe, niraia wa Mali, amekuwa mkurugenzi mtendaji tangu mwaka 2009 katika idara hiyoyenye makao yake makuu mjini Geneva, Uswisi, ambayo ina wafanyakazi 670 Duniani kote. Lakini pia ameijulisha bodi yaUNAIDS katika mkutano huo kwamba kikao cha June, 2019 kitakuwa kikao chake cha mwisho.