28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Waziri aagiza mhandisiapangiwe kazi nyingine

NA OSCAR ASSENGA, PANGANI

NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Profesa Kitila Mkumbo,kumtafutia kazi nyingine, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Pangani, Novath Wilson,kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo miradiya maji wilayani humo na kusababisha  wananchi kukosa huduma hiyo kwa wakati.

Hayo yamesemwa juzi wakati waziara ya siku mbili mkoani Tanga  na Waziri Aweso alipotembelea miradi mbalimbaliya maji inayotekelezwa wilaya ni humo na kutokuridhishwa nayo kutokana nautekelezaji wake kuwa chini ya kiwango, hatua iliyomlazimu kuzivunja baadhi ya kamati za usimamizi wa maji.

Licha ya mhandisi huyo kutoa sababu mbalimbali ya baadhi ya miradi kukwama kutoa maji, Waziri alionyeshwa kutokuridhishwa na majibu hayo kutokana na baadhi ya maelekezo aliyokuwa akimpa ili kuweza kukabiliana na changamoto juu ya miradi hiyo.

“Nimekuita mara ngapi wizarani,tena nikakukutanisha na viongozi wengi labda watakusaidia na kilamara nakupigia simu lakini bado unaonekana si mtendaji wa kazi, sasa nitamwambia katibu mkuu wetu akutafutie kazi sehemu nyingine lakini si hapa Pangani,” alisema Aweso.

Alisema ni jambo la ajabu,ikiwa Serikali inapambana kutenga fedha kwa ajili ya kuwakomboawananchi na tatizo la maji huku baadhi ya watendaji wa Serikali wakishindwa kusimamia vema miradi hiyo na kupelekea wananchi kuichukia Serikali yao.

Awali akijibu hoja, alisema sababu za mradi huo uliotekelezwa kwa zaidi ya Sh milioni 260 kuwa chini ya kiwango, alisema mradi huo ulimalizika machi 2013 na una miaka mitano tangu kukamilika kwake.

Alisema mradi huo unaendeshwana jumuiya ya watumia maji ambayo iliundwa kwa mujibu wakisheria na ndiyo inayoendelea kusimamia mradi huo ambao kuna takribanimita 1,500 kuelekea Kijiji cha Madanga ambapo mabomba yake yalionekana kuchakaa.

Alieleza kwamba, mradi huo una njia mbili za kuelekea Jaira na Madanga lakini kuna uchakavu wa miundombinu ambapo jumuiya iliyopo haikukusanya fedha ili kuwezakufanya ukarabati na ndiyo sababu ya eneo hilo kukosa maji muda wote.

Alishangazwa na mahitaji yamabomba hayo kwa urefu wa mita hizo 1,500 ambayo ni kiasicha shilingi milioni 3 kwa ajili ya bomba za nchi mbili huku jumuiya hiyoikiwa haina hata shilingi kumi jambo lililomtia wasiwasi waziri.

“Mradi wa shilingi milioni 260 na leo hakuna hata shilingi kumi na hakuna maji maana yake wananchi hawa na maji na kila kitu mnatoa majibu ya hakuna mradi huu unaweza ukafa na wananchi wakakosa maji, suala hilisitalivumilia,” alisema.

Wakati huo huo amemwagiza Katibu Mkuu kuhakikisha Mkandarasi wa Kampuni ya Koberg ConstructionLtd, anayetekeleza mradi mkubwa wa maji toka Pongwe jijini hadi wilayani Muheza, analipwa fedha kwa wakati ili kumwongezea ufanisi wa kazizake.

Akizungumzia mradi huo,Mhandisi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Tanga -Uwasa),Salum Hamisi, alisema mkandarasi anayesimamia mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 yupo katika asilimia 50 huku akikabiliwa nachangamoto ya fedha ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake, MkurugenziMtendaji wa Maji Tanga (Uwasa), Mhandisi Jofrey Gerald, alisema ziaraya Naibu Waziri ina manufaa kwa wananchi hasa baada ya kutembelea baadhi ya miradi na kubaini baadhi ya changamoto huku baadhi ya kamati zikionekana kutofanya vizuri nakuchukuliwa hatua.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles